Luke 16:19-24

19 a“Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, ambaye aliishi kwa anasa kila siku. 20 bHapo penye mlango wake aliishi maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima. 21 cHuyo Lazaro alitamani kujishibisha kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani kwa yule tajiri. Hata mbwa walikuwa wakija na kuramba vidonda vyake.

22“Wakati ukafika yule maskini akafa, nao malaika wakamchukua akae pamoja na Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa na akazikwa. 23Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake. 24 dHivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’

Copyright information for SwhKC